NDAKI
YA MTAKATIFU AGUSTINO TANZANIA
KITIVO
CHA SANAA NA ELIMU
IDARA
YA KISWAHILI
KOZI
: SINTAKSIA YA KISWAHILI
MSIMBO
: SW 311
INAWASILISHWA
KWA : PROF. KAHIGI
INAWASILISHWA
NA : KIKUNDI CHA ENLIGHTENMENT (BAED III)
AINA
YA KAZI : KAZI YA KIKUNDI
TAREHE
YA KUWASILISHA : 01/ O2/ 2016
WASHIRIKI
NA | MAJINA | NA, YA USAJILI | SAHIHI |
1 | GASSA RAJABU | BAED III 43062 | |
2 | ADAM DAUDI | BAED III 42862 | |
3 | CHANGWE MADUNYA C. | BAED III 42961 | |
4 | DIPLONIA DAVID | BAED III 43002 | |
5 | KITALY MARIA PIUS | BAED III 43243 | |
6 | MASALU PHILEMON BENARD | BAED III 43374 | |
7 | MAYENGO ALPHA H. | BAED III 43404 | |
8 | MKWAMA ELFRIDA | BAED III 43478 | |
9 | MSEMO ROBERT | BAED III 43520 | |
10 | NARIA ADELINA J. | BAED III 43609 | |
11 | NDUMIWE ELISHAFATI J. | BAED III 43618 | |
12 | NGELELA HERMAN | BAED III 43623 | |
13 | SANGA AGATHA L. | BAED III 43745 | |
14 | SHABANI HIDAYA | BAED III 43761 | |
15 | STANLEY ZEPHANIA K. | BAED III 43803 | |
16 | SUGA SAYI D. | BAED III 43807 | |
17 | SLAQWE NAWE SAREA | BAED III 43877 |
SWALI:
Sarufi miundo virai inatofautianaje na Sarufi geuzi?
Maana ya
sarufi
Kihore
na wenzake (2008) wakimnukuu Gaynor (1968:88) wanaeleza kuwa sarufi
ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria, kanuni na matumizi
yake ambayo kwa kawaida hukubalika kwa watumiaji wake.
Massamba
na wenzake (2009:31) wanaeleza kuwa sarufi ni kanuni, sheria au
taratibu za uchambuzi zinazotawala lugha.
Saluhaya
(2010:72) anadai kuwa sarufi ni kanuni, sheria au taratibu
zinazotawala lugha katika matumizi yake ambayo hujumuisha matamshi,
maumbo, miundo na maana. Taaluma hii husisitiza kanuni zitumikazo
katika uchambuzi wa lugha katika viwango vinne vilivyotajwa hapo juu.
Tofauti ya kimaana
Sarufi miundo virai
Hiki
ni kitengo cha sarufi geuza maumbo zalishi ambacho hujikita katika
matumizi ya sheria chache kuzalisha sentensi nyingi zisizo na kikomo
ambazo zina usarufi na hata zile ambazo hazijawahi kutungwa(Matinde,
2012:233).
Sarufi
miundo virai ni mkabala wa kuchambua lugha kwa kuigawa sentensi
katika virai vinavyoiunda na kasha kuvichanganua zaidi hadi kufikia
neon moja moja lililokiunda kirai.
Sarufi
Geuzi
Sarufi
geuzi ni utaratibu wa kubadili maumbo ya maneno kuwa maumbo mengine
kwa kufuata kanuni maalumu. Sarufi hii hujengwa kwa wazo kwamba
katika lugha kuna sentensi ambazo huwa ni za msingi, ambazo kutokana
na kaida mahususi sentensi zingine huweza kuzalishwa na sentensi hizo
(Matinde, 2012:231). Ugeuzaji huu huathiri muundo wa sentensi na wala
si maana ya sentensi. Kwa mfano;
(a) John amemchapa Bigile.
(b) Bigile amechapwa na John.
Hivyo
basi, ugeuzaji ni mbinu ya kisarufi ambayo hutumiwa katika sarufi
geuza maumbo zalishi kuzalisha sentensi lukuki kwa kufuta sheria au
kanuni maalumu.
Kwa
mujibu wa Habwe na Karanja (2007), Matinde, (2012) wanaonesha
utofauti uliopo kati ya sarufi miundo virai na sarufi geuzi kama
ifuatavyo:
Tofauti
katika maana, sarufi geuzi maumbo ni utaratibu wa kubadili maumbo
kuwa maumbo mengine kwa kufuata kanuni maalumu. Ilhali sarufi miundo
virai ni kitengo cha sarufi geuzi maumbo zalishi ambacho hujikita
katika matumizi ya sheria chache kuzalisha sentensi nyingi zisizo na
ukomo.
Tofauti
katika uchanganuzi wa sentensi, sarufi geuzi huweza kuchanganua
sentensi zenye maumbo tofauti. Kwa mfano sentensi sahili, changamano
au ambatano ilhali sarufi miundo virai hujikita katika kuchanganua
sentensi sahili peke yake.
Mfano;
Rajabu ni mwana wangu.
Tofauti
katika uchopekaji wa viambajengo, sarufi geuzi huweza kuchopeka
viambajengo katika sentensi na kuifanya sentensi hiyo kuwa tenda au
tendwa. Kwa mfano, sentensi ya kauli ya kutenda inapogeuzwa na kuwa
katika hali ya kutendwa kuna elementi ambazo huchopekwa.
Mfano;
(a) Changwe anampiga mtoto
(b) Mtoto
anapigwa na Changwe.
Hapa
tunaona mofu {-w} na kihusishi {na} huchopekwa katika sentensi
(a) na
kuifanya sentensi hiyo kuwa ya kauli ya kutendwa katika
(b) Ilhali
sarufi miundo virai uchopekaji huo haujitokezi na hivyo kutokuonyesha
mahusiano kati ya kauli tendi na tendwa.
Tofauti
ya waasisi, sarufi geuzi iliasisiwa na mwanasarufi aitwaye Noam
Chomsky (1957) ambaye anadai kuwa nadharia hii ya sarufi geuzi
ilizuka ili kurekebisha taratibu za sarufi za awali. Yeye alidai kuwa
sarufi za awali hazingeweza kuonyesha kuwa sentensi ya kauli ya
kutenda na ile ya kauli ya kutendwa zinatokana na muundo mmoja wa
ndani.
Pia sarufi za awali hazingeweza kuonyesha mahusiano ya
sentensi zinazotofautiana kwa ndani lakini ambazo zilikuwa na muundo
wan je mmoja.
Kwa mfano; Herman alinunuliwa shati na mwanawe.
Sura
hii ya nje ya sentensi huwa ina sentensi kadhaa katika muundo wake wa
ndani.
Wakati sarufi miundo virai iliasisiwa na Bussmann (1996)
ambaye anafafanua kwamba sheria miundo virai ni sheria zinazoonyesha
mpangilio na ujenzi wa virai katika lugha, hivyo sheria hii huonyesha
kuandikwa tena kwa viambajengo. Sheria kama,
S=
KN+KT.
Inamaanisha
kuwa sentensi inaweza kuandikwa kama Kikundi Nomino kikifuatwa na
Kikundi Tenzi. Wakati mwingine sheria miundo virai huonyesha uhusiano
wa utawazi hivi kwamba nomino hutawala Kikundi Nomino (KN). Kwa mfano
sentensi kama; Amina ni mke wangu.
Suala
la msingi ambalo wanaumuundo walisisitiza ni kutazama na kuchunguza
lugha kisayansi. Hapa walisema kuwa masuala ilibidi yachunguzwe kwa
uwazi na kuonyesha vitu, kategoria na elementi kwa uwazi zaidi.
Ilhali sarufi geuzi hueleza ujuzi wa lugha ambao msemaji mzawa anao
unaomwezesha kutumia lugha. Huu ni ujuzi wa kutunga sentensi kwa njia
iliyo sahihi na vilevile namna sahihi ya kutamka na kueleza maana za
maneno na sentensi. Mfano mmilisi wa lugha ya Kizinza anaweza kutunga
sentensi zinazoeleweka na kutamka maneno ya lugha hiyo kwa usahihi
kabisa.
Kwa
ujumla, sarufi miundo virai na sarufi geuzi hufanana sana katika
kuchunguza miundo ya lugha husika japo katika utendaji wake
hujitokeza baadhi ya tofauti ambazo husababisha nadharia hizi za
sarufi miundo kutofautiana katika vipengele kadha wa kadha kama vile
uchopekaji wa viambajengo, maana zake pamoja na mfumo wa namna ya
kuchanganua sentensi.
MAREJELEO
Habwe,
J. & Karanja, P. (2004). Misingi
ya Sarufi ya Kiswahili.Nairobi:
Phoenix Publishers.
Habwe,
J. & Karanja, P. (2007).
Misingi ya Sarufi ya Kiswahili.Nairobi:
Phoenix Publishers.
Kihore,
Y.M. na wenzake. (2008). Sarufi
Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Sekondari na Vyuo.
Dar es Salaam: TUKI.
Massamba,
D.P.B na Wenzake (1999). Sarufi
Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA); Sekondari na Vyuo.
Dar es Saalam: TUKI.
Matinde,
R.S. (2012). Dafina
ya Lugha, Isimu na Nadharia; Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo
Vikuu.
Mwanza: Serengeti Educational Publishers (T) LTD.
Saluhaya,
M.C. (2010).
Nadharia ya Lugha Kidato cha Tano na Sita.
Dar es Salaam: CHILDREN EDUCATION SOCIETY (CHESO).
Hii ni kama kumbukumbu kwa wanakikundi ambao karibu kazi zote wao ndio waliotoa mchango mkubwa .......
NAWAPENDA SANA
MUNGU AWABARIKI WANA ENLIGHTENMENT 2013/2016 .
No comments:
Post a Comment