MKONDO WA KIMAPINDUZI
Kwa muujibu wa Madumulla (2009:69) anasema ni mkondo ambao hujadili
matatizo ya kisiasa ikiwa na mwelekeo fulani wa kuleta mabadiliko ya
kisiasa na jamii. Ni mkondo unaozungumzia mabadiliko ya kisiasa
katika jamii, wnanchi wakitaka kupigania haki zao na kuleta
mabadiliko katika jamii.
Sababu zakutokea kwa mkondo huu
ni mabadiliko ya
Kisiasa, watu kutaka kudai haki zao na ulitokea katika miaka ya
sabini.
Riwaya zilizoandikwa wakati huo ziliongelea mnyonge kuchukua silaha
kupambana na mwenye nguvu ili kupigania haki zao, mkondo huu ulikuwa
umekusudia kuleta usawa na haki katika jamii. Mfano: wa riwaya katika
mkondo huu ni kuli iliyoandikwa
na Shafi Adam Shafi, Nyota
ya Rehema, Kasri ya Mwinyifuad, Giza katika Nuru, Utengano
iliyoandikwa na A.J. Saffari,
Vuta n'kuvute
iliyoandikwa na Mohammed.
S. Khatibu.
MAUDHUI YA RIWAYA KATIKA MKONDO WA KIMAPINDUZI.
Binadamu hutazamwa kama zoon politikon,
yaani mnyama wa kisiasa, Mnyama mwenye uwezo wa kupatana.
Baadhi ya riwaya kuweka mkazo katika itikadi
kama msingi au dira ya kuielekeza jamii.
Husisitiza umuhimu wakuwa na msimamo na
mwelekeo.
Kwa mfano: Katika kitabu cha vuta n'kuvute mwandishi ametumia
muhusika Denge kuonesha msimamo
kwa kutetea haki ya watu weusi dhidi ya watu weupe au wakoloni. Vile
vile katika kitabu cha Dunia mti mkavu –
kilichoandikwa na Said Mohamed,
amewatumia wahusika Mashaka na Bakari
kuonesha jinsi walivyopigania haki za uma. mfano: kuiba
chakula kwaajili ya uma.
Umuhimu wa uma kuleta mapinduzi.
Kwa mfano katika kitabu cha vuta nikuvute kilichoandikwa na Shafi
Adam Shafi; ametumia mhusika Denge na wahusika wengine
kama Chande, Mambo na Yasimine walivyoweza kuandaa vipeperushi
mbalimbali kwaajili ya kuelimisha jamii, ili kuiondoa madarakani
serikali ya kikoloni kwa ajili ya ukombozi wa mtu mweusi.
Usawa wa binadamu.
Hapa waandishi mbalimbali
wanajaribu kuonesha jinsi binadamu wanavyotakiwa kuhusiana na
kushirikiana katika jamii bila kujali tofauti zao.
Mfano; Katika kitabu cha takadini;
mwandishi amemtumia mhusika Sekai
alivyojaribu kupigania haki ya walemavu wa ngozi, hasa kumtorosha
mwanae.
Mapinduzi kupatikana hata kwa njia ya mapambano.
Kwa mfano: Katika kitabu cha vuta nikuvute kilichoandikwa na Shafi
Adam Shafi. Mwandishi
amemtumia mhusika Denge kuonesha
jinsi ambavyo amejitoa mhanga kupamabana katika kuleta mapinduzi. Hii
inadhihirika pale ambapo mhusika Denge
apambana hadi kufungwa gerezani.
Demokrasia ya uma. Riwaya nyingi za kimapinduzi zinasisitiza
sana uwepo wa demokrasia ya kauli kwa jamii husika. Hii ina kuwa
usawa na haki uzingatiwe kwa wanajamii bila kujali matabaka
yao.
Kwa mfano katika kitabu cha adili na
nduguze, kilichoandikwa na Shabani
Robert. aliyewatumia wahusika manyani
kuonyesha jinsi walivyokuwa wakihangaika kudai haki zao, wao kama
tabaka la chini na majini wakiwa tabaka la juu. Hivyo manyani
walikuwa wakidai haki, na usawa toka kwa majini (wakoloni).
muundo wa
mbinu katika mkondo wa kimapinduzi
Wahusika ambao wanatoa mwanga kuhusu mwelekeo na wenye msimamo
wa kuelewa hali ya matatizo ya kijamii, kihistoria, kisiasa na
kiuchumi.
Kwa mfano: katika kitabu cha takadini
kilichoandikwa na Ben
Hanson mwandishi amemtumia muhusika Sekai
amefanikiwa kuonesha mwelekeo kuwa mulemavu wa ngozi sio kwamba
atazaa walemavu wa ngozi.
Hujaribu kuepuka mawazo mufilisi
Mawazo hayo ni kama vile mapenzi, ujamabzi
na mijadara kuhusu Mungu. Kwa mfano; katika kitabu cha
Vuta nikuvute, mtunzi amemtumia muhusika
Denge kuonyesha kuepuka mawazo mufilisi. Denge alikataa
kujihusisha kimapenzi na Yasmini
vile vile mwandishi katika kitabu hiki hajazungumzia suala la
ujambazi na mijadala kuhusu Mungu.
Lugha huwa rahisi inayoweka matatizo bayana bila kificho
Kwa mfano; katika kitabu cha Watoto wa Mama Ntilie,
kilichoandikwa na Emmanuel Mbogo ametumia lugha rahisi inayoweka wazi
matatizo ya kijamii kama vile umasikini, uonevu na unyanyasaji.
Suluhisho kwa kawaida ni la kijamaa au kisoshalisti katika riwaya za
kimapinduzi.
MAREJELEO:
Madumulla, J. S (2009) Riwaya ya Kiswahili, Nadharia, Historia na
Misingi ya uchambuzi. Dar es Salaam Tanzania: Mture Educational
publishers Ltd.
Kitabu cha vuta n'kuvute
Kitabu cha takadini
Kitabu cha Watotot wa mama ntilie
Kitabu cha dunia mti mkavu
Adili na nduguze
No comments:
Post a Comment