Tuesday, July 5, 2016

Ulinganishaji wa tanzu za fasihi simulizi ya kiswahili na ile ya kibantu.

Ulinganishaji wa fasihi simulizi ya kiswahili na ile ya kibantu 
                    
a)       Mifano ya methali katika lugha ya Kizinza
  1. Kizinza : Ente elikwilagula, kukamwa amata galikwela.
Kiswahili : Ng’ombe mweusi kukamuliwa maziwa meupe.
  1. Kizinza : Ibhale kumela, litene muzi.
Kiswahili : Jiwe kuota bila mzizi.
  1. Kizinza : Enzemu kuzala, etene mukwata.
Kiswahili : Mgomba kuzaa bila mume.
  1. Kizinza : Enkoko kwoncha, etene mabhele.
Kiswahili : Kuku kunyonysha bila matiti.
  1. Kizinza : Enzoka kulibata, etene magulu.
Kiswahili : nyoka kutembea bila miguu.


  1. Vitendawili. Mifano ya vitendawili katika lugha ya Kizinza
  1. Kizinza : Ntela enchitasimbuka…………. (ensimbazi).
Kiswahili : Napiga kisichostuka…………… (giza).
  1. Kizinza : Ndibata nechitandindila………… (omuhanda)
Kiswahili : Natembea na kisichinisubuli ………. (njia)
  1. Kizinza : Tinyihamo omo tindya…………….. (amahiga)
Kiswahili : Nitowapo moja huwa sili……….. (mafiga)
  1. Kizinza : Ahotulyaha omukama noha…………(omulilo)
Kiswahili : Tulipo hapa mfalme ni nani……….... (moto)
  1. Kizinza : Naho mwanawe elabha…………. (ihulu lyenzu)
Kiswahili : Lakini wewe mtoto huangalia………….. (tundu la nyumba)
(c) Nyimbo. Mfano wa wimbo wa harusi katika lugha ya Kizinza
OLUZINA LWOBWENGA
Yahuwee yahuwee yahuwee abhalonzi babayo,
Kuswelwa omuseza mubhi amuhanda omwibembeza,
Tibabhuza ogwo ni balo imbagambila nomukozi akola ahamuka,
Yahuwee yahuwee yahuwee abhalonzi babayo x2
WIMBO WA HARUSI
Jamaniee jamaniee jamaniee watafutaji huwa wapo,
Kuolewa na mwanaume mbaya njiani unamtanguliza,
Wakikuuliza huyo ni mmeo nawambia ni kijakazi hufanya kazi nyumbani,
Jamaniee jamaniee jamaniee watafutaji huwa wapo
Kamuoa mwanamke mbaya njiani unamtanguliza
Wakiuliza huyo ni mkeo nawambia ni kijakazi hufanya kazi za nyumbani.
Jamaniee jamaniee jamaniee watafuataji huwa wapo x2


  1. Hotuba. Mfano wa hotuba katika lugha ya kikinga
ILITATIZO LYA UVUHAVI PA KIJIJI
Valokholo vanakijiji nditegemela mgemila ilelo ndyemle mbele jinyo ukhocho vevela ilitatizolya uvuhav. Ilikhomela pa kijiji kyawe.
Valokholo vanakijiji, avahenga vakhecho tchovile khame nauzibili uvufa jou tchenga uvukuta kwani khememetuzuile ihtatizo lya uvukhevi pa kijiji kyawe jokhijaga.
Valokholo vanakijiji ifikhuizi tchapakheribu khuomie na matukio kha khudwatcha. Aghivionesa uvuhavi pa kijiji kyawe moja ya mambo hayo ni
Ukujagha khwa vana; valokholo vana kijiji, nditeghemela voni. Mpolike etaarifa ja ukhuijaghakwa vana mu mazingira kha khutatanisha. Umwana wa Mgogolo Chimbuzi akhojaghile akhepindi chya khutchunga, umwana wa mkokolo Ngolole akhaagile pa kisima pamoja kno mwana wa mkokolo Luhenda akhojagila ikhepindi hela kya. Kuhegala inyagala.
Khuvonekha khwa emisukule; valokholo vanakijiji, pa kijiji kyawe pavie na amatatizo gha kuonekha kwa avanu avsue khatale, thotsi avana view. Uvuvakhamila khosyole vakhambwene u bwana Luhelwa Uvakhasue e miaka khadatu igigendile, tena e wiki eji ghendile u mama Luchululu akhevonikha pa njia panda ja khuluta pa khesima akhielenga avanu.
Elitatizo lya khogona panzi; valokhelo vanakijiji avahenga khogona panzi valokhilo vanakhejiji avahenga vakhtcho vile ovibela panonu pavivi pivivi pikhomwelanga. Vanakhejiji tuvonekha natunogwa avanavawe vasome esyole basi avamo vame juvikhwendelea khuva va pelwapelwa ekhijiji kyawe jokhikhosa amaendeleo na khuzidiwa na ekhejiji kya Mavanga. Khwani avanu avoviletw khusomesa avana vawe vikhoneswa khonzi kha mibuya khehavi mumbale na lywangwa kipuera na muvivanza.
Vavokholo vanakhejiji, khama onende chifu pa khejiji kyame, khuanza za elelo avanu ovonivomba amamboghe uvuhavi valekhe mara moja khwani umunu ujikwibatwa ighaa uvughalaghela uvyo vywa ukuhani ji homya efrani ya eng’ombe moja ne eligunila lya uvyonga bakho pampja na ukhosema pa kijiji khyawe.
Mwalemi khwa, khumulisa, elisago iyane kwanye, khuvombela mbombo elimenyo iyototchonile elelo hapa mwalemi sana.
TATIZO LA UCHAWI KIJIJINI
Ndugu wanakijiji natumai hamjambo. Leo hii nimesimama mbele yenu kuzungumzia tatizo la uchawi linalokikabili kijiji chetu.
Ndugu wnakijiji, wahenga walisema usipoziba ufa utajenga ukuta kwani tusipodhibiti tatizo la uchawi kijiji chetu kitaangamia.
Ndugu wanakijiji, siku hizi karibuni kumekuwepo na matukio ya kutisha yanayodhihilisha uwepo wa uchawi kijijini kwetu. Matukio hayo ni kama yafuatayo:
Upotevu wa watoto; ndugu wnakijiji, nadhani wote mmesikia taarifa juu ya upotevu wa watoto watatu katika mazingira ya kutatanisha. Mtoto wa mzee Ngolole aliyepotelea kisimani pamoja na mtoto wa mzee Luhenda aliyepotelea wakati alipoenda kukusanya kuni.
Kuonekana kwa vizuka; ndugu wanakijiji, kijiji chetu kimekumbwa na tatizo la kuonekana kwa watu waliofariki zamani. Juzi wanetu walipokuwa wakitoka shuleni walimuona Bwana Luhelwa aliyefariki miaka mitatu iliyopita. Pia wiki iliyopita Mama Luchululu alionekana njia panda ya kwenda kisimani akiwaita watu.
Tatizo la kulazwa nje; ndugu wnakijiji, wahenga walisema mkataa pema pabaya namamwita. Wanakijiji, tunaonekana kwamba hatutaki watoto wetu wapate elimu hiyo wanetu wataendelea kuwa wajinga, hivyo kijiji chetu kitakosa maendeleo na kuzidiwa na kijiji cha Mavanga kwani wanaoletwa kutufundishia watoto wetu wanalazwa juu ya mibuyu, kando kando ya mto Kipewra na viwanjani.
Ndugu wanakijiji nikiwa kama chifu wa kijiji hiki, kuanzia sana wenye tabia hizo za uchawi waache mara moja kwani kwa atakayebainika kujihusiha na jinga huo atatozwa faini ya ng’ombe watano na unga gunia moja. Vilevile licha ya adhabu hiyo, mhusika lazima tumfukuze kijijini kwetu.
Akhsanteni kwa kunisikiliza ombi langu kwenu ni kuzingatia tuliyoyazungumza katika kikako hiki cha leo.
  1. Malumbano ya watani. Mfano wa malumbano ya watani katika lugha ya Kizinza
BHUCHIGULWA
Omwanya gwalofu nokunaga oluganda lwa bayungu na abheriri
Omuyungu : imulila chiha ogu achalikufa tali kunsekelela!
Omwiriri : nobuza chiha nimwe mwavita guku wenyu mbamutina kwobulozi echijiji chona niwe yamwita.
Omuyungu: ha! ha! ha! bhamwita nkahi oguahunile kwonka obhujanja bwenyu twabumannyile imubagambila abantu bhahunile ili mubone emichango leo tikuchangia omuntu alachanga ntutwala yona timukubona nesumani.
Omwiriri : twabamanyile imwita badugu bhetumuze kubakolesa omumashamba genyu, muketa tizibazomo twamsanga omwishamba lya kakawenyu nayembula amapo, tutukwikiliza mpaka mdugu wetu mumusubye muganya timlayanga kakawenyu ntumwihalo ebhicha.
Omuyungu : nemwe mwayebilwe nkokwo mulyaaba lozi, guku wawe akasangwa na sela ahabutuzi, nabakamgambila aite omwana womwe wobuzigezwa nikwo yamugambila ahunile abhantu bazile bhati yafa kumbe tiyafa. Mpa amenzi mulebhe talabha ataganywile.
Omwiriri: amenzi gachi naho nimwe mwatwitila mdugu wetu, lebha watukwilwe ameso kwobulozi.
Omnyunyu : talaba yafa itwenda ente, timlabha mutatulole ntumubaga nakumulya
Omwiriri : mubaletele embwa yabho bhehake
Omungungu : timwakulekile kutuha twakamubagile nokumulya omumeso genyu.
Omwiriri : mutulugile aha bhalozimwe mzende kulya akabwa kenyu
Omunyungu : twabakaza mutakusubhila kubagambila bhandugu bhenyu bahunile.
Twamala
MALUMBANO YA WATANI
Mfano wa kati wa msiba na mazishi yake kati ya ukoo wa bayungu na abheriri
Muyungu : mnalia nini? huyu hajafa mbona anacheka
Mwiriri : unauliza nini? Na wakati nyie ndo mmemuua, tena babu yako mchawi anayeogopwa kijiji kizima ndiye kamuua,
Muyungu: ha! ha! Ha! kauliwa wapi wakati kasinzia tu, na mbinu zenu tumeshazijua mmemwambia asinzie ili mpate mchango ya msiba, na leo hachangii mtuu, na akichangaa tunachukua michango yote, hampati hata sumuni.
Mwiriri : tabia zenu tuazijua mnaua ndugu zetu ili mkawafanyishe kazi huko mashambani kwenu. Mlimuua Tuzibazamo, tukamukuta shambani kwa bibi yako anavuna mahindi. Leo hatukubali mpaka mumfufua ndugu yetu, vinginevyo bibi yako tunamtua shingo.
Muyungu : na nyie mmesahau mlivyo wachawi, babu yako alikutwa anawanga kwa jirani na adhabu yake aliaambiwa amtoe kafara mwanae wa kwanza na ndiyo maana mmemwambia sinzie watu wajue amekufa kumbe hajafa. Lete maji nimunyweshe tuone kama hatokunywa.
Mwiriri : maji ya nini wakati nyie ndiyo mmetuulia ndugu yetu, ona macho yalivyo mekungu kwa sababu ya uchawi.
Muyungu: na kama amekufa tunataka ng’ombe, msipotoa tunamchinja na kumla.
Mwiriri : waleteeni mbwa wao wakafakamie
Muyungu : Msingetoa leo, mngeona tungemchinja na kumla mbele yenu
Mwiriri : tokeni wachawi wakubwa nendeni mkale hicho kimbwa chenu.
Muyungu : tumewakomesha ili msirudie kuwaambia ndugu zenu wasinzie.
Mwisho.
  1. Ngano za usuli. Mfano wa ngano za usuli katika lugha ya Kiha
IJOSI DYI MBUNI NI NGONA
Umcha migani: Ngane imigani…..!
Abhaganigwa : gana………!
Halabhaye, ingona ni mbuni bhali abhagenzi bhakundanye chane. Umwanya wose mbuni agiye kumgezi, yalamlasa muhaliwage ngona kulukuondo atalamwa amazi. Mbuni yalamthamini chane uwo mhali wage. Ingona yadya ibhikoko ni nzebha alikolelo ntiyashobhora kumdya mhali wage imbuni nu musi na umwe. Muwo mwanya imbuni yalabhanye ijosi ligufi hanyuma niyimisi.
Imisi yose ingona yategera ibhikoko bhije ukumwa amazi kuko yolonka ibhilibwa vyage na niyo hali ingeso yage. Aho lelo hali ingeso yage yukwinyegeza mumazi nu kwegela aho ibhikoko hibhili. Aho yarakidarukira igikoko kimwe nu kugifatisha amenyo yage nu kukibhulumlila mmazi kuja kukilila hiyo. Ahaze yalava mmugezi nu kugahrama kulusi ukota izubha hamwe nu mugezi.
Umusi umwe, ingona yalifise inzara chane, uwo musi yalategeye ibhikoko bhize nkimise yose lakini hali umusi mubhi iwage. Nta gikoko na kimwe chaziye ukumwa amazi. Inzara ikomoye yalaifashe ingona ntiyimenye chu gukora.Hiyari muwo mwanya yalamubhonye mgenzi wage mbuni hayaza, ntakundi nukumfata mhali wanje mbuni nukumdya aho ndo kila inzara yinfise, ingona yaliyumviye. Mbuni yalamwegeye umugenzi wage nu kumulamsa nkadyo vyalibhili, abhona umugenzi wage ngona nta shimwe afise nkadyo yali aho hanyuma. Mbuni avuga,
Mbuni : emugenzi wanje ufise iki?”
Ingona : Kuki? (kwi jwii dyi hefo nu dyu bhulushi)
Mbuni : hayambona ata shimwe ubhanye
Ingona : Idyenyo hayelindya chane
Mbuni : Idyenyo?
Ingona : ehe!, ndalindakutegeye uze ulilabhe umbwile nkadyo libhaye.
Mbuni : oooh!, hola chane, nuko lelo asama ndalilabhe.
Ingona : ehe, mhali wanje ni ndyenyo dya hanyuma nyene.
Imbuni yingije umutwe wage mumunwa wi ngona kulabha idyo dyenyo. Muwo mwanya nyene agizentyo, ingona yahweje ilumya umunwa wage nukwivuta ugusubhira mumazi. Imbuni nayo ilikoilagerageza kwivanamo. Yalagerageje ku nguvu zage zose gusubhila hanyuma. Aholelo imbuni hiyaliyivuta kusubhila inyuma ni ngona yaliyivuta kusubhila mumazi. Uko kuvutana kwaledeleyeje ukishikila ijosi ndyi mbuni ukwanza kureha. Kwi bahati yisole imbuni yalafanikiwa ukuvanamo umutwe wage mumunwa wi ngona. Mbuni yahweje nyiruka ugusubhira mwi poro ni josi dyage dyaweje lireha. Ubhugenzi bwage ni ngona bwafyiliye uwo musi na kuanzila ngaho imbuni yahweje ibhana ijosi lilishe mpaka ntya.
SHINGO YA MBUNI NA MAMBA
Fanani: hadithi!... Hadithi!.....
Hadhira : Hadithi njoo utamu kolea!.....
Hapo zamani za kale mbuni na mamba walikuwa marafiki wakubwa sana. Kila wakati mbuni alipokwenda mtoni alimsalimia mamba kwa mapenzi makubwa kabla ya kunywa maji. Mbuni alimthamini sana rafiki yake huyo. Ingawa mamba hula wanyama na ndege ila yeye hakuweza kumdhuru rafiki yake mbuni hata siku moja. Katika kipindi chicho mbuni alikuwa na shingo fupi tofauti na ilivyo sasa.
Kila siku mamba husubiri wanyama waje kunywa maji ili apate mlo wake kama kawaida yake. Hii ilikuwa ni kawaida yake kujificha majini na kuwasogelea wanyama hadi walipokuwa wanakunywa maji. Hapo alimrukia mnyama mmoja hadi walipokuwa wanakunywa maji. Hapo alimurukia mnyama mmoja na kumng’ata kwa meno yake na kumvuta majini kwenda kumlia huko. Baada ya shibe hutoka majini na kujilaza mcahngani kuota jua karibu na mto.
Basi, siku moja mamba alikuwa na njaa, siku hiyo alitegemea wanyama waje kama kawaida yake. Lakini kwa bahati mbaya hakuna mnyama hata mmoja aliyekuja kunywa maji. Njaa ya ajabu ilimshika mamba asijue cha kufanya. Alipokuwa katika hali hiyo alimuona rafiki yake mbuni akija. Sina njia nyingine isipokuwa kumshika mbuni na kumla ili kuzima njaa iliyonishika, mamba aliwaza. Mbuni alimsogelea rafiki yake na kumsalimia kama kawaida na kutambua kuwa mamba hakuwa na furaha yake ya kawaida. Mbuni nasema,
Mbuni : “Rafiki yangu mamba una nini?”
Mamba : kwa nini? (kwa sauti ya chini na unyonge)
Mbuni : Naona huna raha kabisa
Mamba : Jino linanisumbua sana
Mbuni : Jino?
Mamba : Ndiyo, nilikua nilikuwa nimekusubiri tu uniangalie na kuniambia hali ya jino
Mbuni, : oooh! Pole sana, basi fungua kinywa niangalie.
Mamba : ndiyo rafiki yangu jino la mwisho kabisa,
Mbuni alikiingiza kichwa chake ndani kuliangalia jino la rafiki yake mamba. Mara tu alipofanya hivyo, mamba alikifumba kinywa chake na kuanza kujivuta kurudi majini. Mbuni naye alijitahidi kufurukuta. Alijitahidi kwa nguvu zake zote kurudi nyuma.Kadri mbuni alivojivuta kuelekea nyuma ndivyo mamba alivyojivuta kuelekea majini kinyumenyume. Mvutano huu uliendelea mpaka shingo ya mbuni ikawa inarefuka. Kwa bahati mbuni alifanikiwa kufurukuta na kukitoa kichwa chake kwenye kinywa cha mamba. Mbuni alitimua mbio akirudi zake porini. Urafiki wake na mamba iliishia siku hiyu na tangua hapo mbuni akawa na shingo ndefu.


  1. Kisasili. Mfano wa kisasili katika lugha ya Kisukuma
SHANDYO SHA NYANZA YA NG’WANZA.
Nganji : Kalagu...
bhadegeleki :Kize!
Oliho ngikulu, olinang’witunja okwe na bhaniki bhabhili. Ungikulu ng’wenuyu ofugage ndilo mluzoga ulolwikalage guchumba lukundikijije. Indilo shinisho ojitumilage giti ikubhi ulushigu bhakumbulaga ndilo. Bhaadaye ung’witunja utola nkima, ungikulu ubhiza opandika ng’winga nanhwe aladamanile imijilo ya hakaya yiniyo, ubhiza ungikulu wandya guntongela imijilo ya henaho ili imane nanhwe ung’winga.
Lushigu lumo ungikulu na bhaniki bhakwe bhamla guja kujusena nhwi ng’wipolu ja guzugila, ungikulu ubhiza onagija ung’winga azuge shagulya sha limi. Ung’wila alazubhule indilo umluzoga ila asizibha ugulukundikija. Nhana ung’winga wandyaguhyagija gupyagula numba na goja shiseme sha kuzugila. Bhaada ya henaho uja gujuzubhula ndilo umluzoga, ahoomala guzubhula wibha ugukundikija ahaluzoga uja gujendeleya na milimo yakwe ya guzuga bhila gwizuka giki adalukundikijije uluzoga.
Ogimanila obhona minzi alokala umnumba andya gusambala pye ilibala lya heneho ahakaya. Yeeeeh! Wizuka giki adalukundikijije uluzoga lo ndilo. Wandya gutula ng’wano, pye abhanzengo bhandya gushangaa ugubhona minzi okalaga pye ilibala, bhamla bhuling’wene andye gwibhegeja gwikombola inholo yakwe ila nduhu uyo agafanikiwa.
Ungikulu na bhaniki bhakwe bhalinga ugunhwi bhushangaa ugubhona pye unzengo gobho gokala minzi na angi atali ongezeka kusambala. Uyomba ungikulu, “Hiiiiii!, ung’winga one wibhaga ugukundikija ahaluzoga lone, otumala gete”. Ahoomala kuyomba shinisho, ung’weyi na bhaniki bhakwe bhutibhila na gutibhila pye abhose. Lyubhiza lyokala minzi pye ilibala. Ishinisho hi shandyo sha Nyanza ya Ng’wanza.






ASILI YA ZIWA VIKTORIA
Fanani: Hadithi hadithi...
Hadhira :Hadithi njoo; tena njoo; na utamu kolea.!
Hapo zamani za kale palikuwepo na bibi mmoja ambaye alikuwa na mtoto mmoja wa kiume na wawili wa kike. Huyu bibi alikuwa akifuga samaki kwenye mtungi ambao ulikuwa umewekwa chumbani na haufunguliwi ovyoovyo. Samaki hao walitumika kama mboga siku bibi akijisikia. Baada ya mtoto wake wa kiume kuoa mke, bibi akawa amepata mwali ambaye hakufahamu sheria na taratibu za familia ile hivyo bibi huyu akawa na jukumu la kumwelekeza na kumfundisha taratibu za nyumbani pale.
Siku moja bibi pamoja na binti zake walipanga safari ya kwenda kutafuta kuni za kupikia, hivyo akamwachia mwali wake jukumu la kuandaa chakula cha mchana ambapo alimwagiza kuwa achukue samaki kutoka kwenye mtungi wake lakini asisahau kufunika. Mwali akaanza harakati za kufanya usafi wa nyumba pamoja na kuosha vyombo vya kupikia. Baadaye mwali akaenda kuchukua samaki kwenye mtungi na alipomaliza tu kuchukua wale samaki aliohitaji akasahau kuufunika ule mtungi wa samaki. Akaendelea na kazi zake za mapishi bila kukumbuka kama hajafunika mtungi.
Ghafla akaona maji yanajaa ndani ya nyumba na hatimaye yakazidi kusambaa eneo lote la pale nyumbani. Looo! Alikumbuka kuwa hakuufunika ule mtungi wa samaki. Akaanza kupiga kelele , watu wote pale kijijini wakashangaa kuona maji yanazidi kutanda kila sehemu jambo ambalo liliwafanya waanze kuhangaika kuzinusuru nafsi zao bila mafanikio yoyote.
Bibi na binti zake wakiwa wanatoka huko kuokota kuni walishangaa kuona eneo lote la kijiji chao limejaa maji na bado yanazidi kuongezeka. Yule bibi akasema, “ Oooooh! mwali wangu hakuufunika mtungi wangu, ametuteketeza”. Baada ya kusema hivyo, yeye na binti zake wakatitia wote na eneo lote likawa limejaa maji. Huo ndio mwanzo wa kutokea kwa Ziwa Viktoria.




  1. Maigizo. Mfano wa igizo la matambiko katika lugha ya Kisukuma
TAMBIKO LYA KUMALA MAKOYE
(Bhanazengo bhalibhonekana bhatebhayegu, bhuli ng’wene widimaga itama. Untemi alihang’wakwe atumanaga isho shilendelea).
Ng’wanazengo 1: Bhabehi nibholi amakoye gakwilile geke umzengo gwise? Mbula nduhu, mitugo jilegaiwa minze, shiliwa nduhu, nange hung’wisho go wolelo!
Bhanazengo bhose: (bhohaya) ilidakilwa tuntume njumbe ng’wa Ntemi akang’wele pye aya na tumane ung’wei aliganika ginehe.
Njumbe: (Wingila ng’wa Ntemi na kwandya mahoya). Nkulu Ntemi Mashimba, gite umo ulibhonela amakoye umzengo gwise gatushilaga, ki shandyo sha genaya pye?
Ntemi: Nunene natumanaga, kulwanguno haho obyalila unke wane mabhasa bhuyegu bhone bhushila.
Nshauri: Nkulu Mashimba, ilidakilwa tukamone Ntabiri atulokeje shandyo sha genaya pye, naki twite tulikane nago.
Ntemi: Iganiko lya wiza. Tumaga bhayanda bhakang’witane u Ntabiri (Lunduma).
Ntabiri: Niza nkulu Ntemi, nazunije ukukwambilija kulwanguno bhugota wa henaha bhudo no ila bhudakile bhuzunya wako.
Ntemi: Nazunije. Natuyegaga na makoye genaya umzengo gwane.
Ntabiri: Isho shilekoya habhana bhako mabhasa gite umo umanilile amasamva gise gatadakile mnho oseose umzengo gwise kubyala mabhasa. Ulu ulidaka gashile amakoye genaya Doi alidakilwa afunywe akaponywe mwiporu lya Giningi. Ugwenuyo gukubhi ng’wisho gwa makoye pye.
Ntemi: Nke wane mochage u Doi ung’wine Lunduma, ubhebhe ushoke mnumba abhise tuje nahwe ung’wiporu.
(Aho bhashika ukwiporu, Lunduma umocha u Doi na kuyomba mihayo ya kulomba kuzuniwa kafara yabho. Umocha na kunaja higolya ya liwe litale na kunsesebhela mininga ga mbuli yape. Aho wamala ubhahamilija pye abhanazengo kwinga bila kugaluka numa. Aho bhamala ukutambika pye makoye gushila hangi nubhuyegu bhushoka hange umzengo go Nyaluhande).




TAMBIKO LA KUONDOA MATATIZO
(Wanakijiji wanaonekana wakiwa hawana furaha, kila mmoja kashika shavu. Mtemi yupo kwake akiwa hajui nini kinaenedelea).
Mwanakijiji 1: Jamani mbona matatizo yamekithiri katika kijiji chetu? Mvua hainyeshi, mifugo inakosa maji na malisho, vyakula hakuna, au ndo mwisho wa dunia!
Wanakijiji wote: (wanadakia) inabidi tumtume mjumbe kwa Ntemi akamweleze haya yote na tujue yeye anafikiria nini.
Mjumbe: (akibisha hodi kwa Ntemi na kuanza mazungumzo). Mtukufu Mtemi Mashimba, kama unavyoona matatizo katika kijiji chetu hayaishi, nini chanzo cha haya yote?
Mtemi: Mimi mwenyewe sijui, maana tangu mke wangu ajifungue mapacha furaha yangu ilidumu kwa muda mfupi.
Mshauri: Mtukufu Mashimba, inabidi tukamuone mtabiri Lunduma atuonyeshe chanzo cha haya yote na nini tufanye ili kuepukana nayo.
Mtemi: Wazo zuri. Tuma vijana wakamuite Lunduma.
Lunduma: Ndio mtukufu, nimeitika wito wako na niko tayari kukusaidia kwani tatizo hili suluhisho lake ni dogo sana ila linahitaji utayari wako.
Mtemi: Niko tayari. Hata mimi sifurahishwi na matatizo katika kijiji changu.
Lunduma: Tatizo kubwa ni hawa watoto wako mapacha kwani kama ujuavyo mizimu ya mababu zetu haikubali mtu yeyote katika kijiji chetu kuwa na watoto mapacha. Hivyo inabidi Doto atolewe kafara kwa mizimu ya kijiji katika msitu wa Gingili na huo utakuwa mwisho wa haya yote.
Mtemi: Mke wangu mbebe Doto umkabidhi kwa Lunduma harafu wewe urudi ndani sisi twende naye msituni kwa ajili ya kukamilisha shughuli hii.
(Walipofika porini waliekea kwenye jiwe kubwa wakiwa wamechukua na mbuzi kwa ajili ya kupata damu itakayoandamana na kafara ya Yule mtoto. Mtabiri anambeba Doto na kunena maneno yanayoshiria kuomba kukubaliwa kwa kafara yao. Baadae anamnyanyua Doto na kumweka juu ya lile jiwe kubwa, kisha inaletwa damu ya Yule mbuzi na kunyinyiziwa Doto mwili wote akiwa am ekarishwa pale kwenye jiwe. Baada ya hapo mtabiri anawaamuru wanakijiji wote waliokuwepo pale waondoke lile eneo bila kugeuka nyuma kama ulivyo utaratibu wao kila wamalizapo tambiko. Baada ya kurejea nyumbani, hali ya hewa kijijini pale inabadilika na kuwa shwari kabisa, kwani wingu zito linatanda kuashiria uwepo wa mvua. Furaha inarejelea katika kijiji cha Nyaruhande).


Tofauti kati ya Sarufi miundo virai na Sarufi geuzi?

SWALI: Sarufi miundo virai inatofautianaje na Sarufi geuzi?
Sarufi ni nini ?
Kihore na wenzake (2008) wakimnukuu Gaynor (1968:88) wanaeleza kuwa sarufi ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria, kanuni na matumizi yake ambayo kwa kawaida hukubalika kwa watumiaji wake.
Massamba na wenzake (2009:31) wanaeleza kuwa sarufi ni kanuni, sheria au taratibu za uchambuzi zinazotawala lugha.
Saluhaya (2010:72) anadai kuwa sarufi ni kanuni, sheria au taratibu zinazotawala lugha katika matumizi yake ambayo hujumuisha matamshi, maumbo, miundo na maana. Taaluma hii husisitiza kanuni zitumikazo katika uchambuzi wa lugha katika viwango vinne vilivyotajwa hapo juu.
Sarufi miundo virai
Hiki ni kitengo cha sarufi geuza maumbo zalishi ambacho hujikita katika matumizi ya sheria chache kuzalisha sentensi nyingi zisizo na kikomo ambazo zina usarufi na hata zile ambazo hazijawahi kutungwa(Matinde, 2012:233).
Sarufi miundo virai ni mkabala wa kuchambua lugha kwa kuigawa sentensi katika virai vinavyoiunda na kasha kuvichanganua zaidi hadi kufikia neon moja moja lililokiunda kirai.
Sarufi Geuzi
Sarufi geuzi ni utaratibu wa kubadili maumbo ya maneno kuwa maumbo mengine kwa kufuata kanuni maalumu. Sarufi hii hujengwa kwa wazo kwamba katika lugha kuna sentensi ambazo huwa ni za msingi, ambazo kutokana na kaida mahususi sentensi zingine huweza kuzalishwa na sentensi hizo (Matinde, 2012:231). Ugeuzaji huu huathiri muundo wa sentensi na wala si maana ya sentensi. Kwa mfano;
(a) John amemchapa Bigile.
(b) Bigile amechapwa na John.
Hivyo basi, ugeuzaji ni mbinu ya kisarufi ambayo hutumiwa katika sarufi geuza maumbo zalishi kuzalisha sentensi lukuki kwa kufuta sheria au kanuni maalumu.
Kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2007), Matinde, (2012) wanaonesha utofauti uliopo kati ya sarufi miundo virai na sarufi geuzi kama ifuatavyo:
Tofauti katika maana, sarufi geuzi maumbo ni utaratibu wa kubadili maumbo kuwa maumbo mengine kwa kufuata kanuni maalumu. Ilhali sarufi miundo virai ni kitengo cha sarufi geuzi maumbo zalishi ambacho hujikita katika matumizi ya sheria chache kuzalisha sentensi nyingi zisizo na ukomo.
Tofauti katika uchanganuzi wa sentensi, sarufi geuzi huweza kuchanganua sentensi zenye maumbo tofauti. Kwa mfano sentensi sahili, changamano au ambatano ilhali sarufi miundo virai hujikita katika kuchanganua sentensi sahili peke yake.
Mfano; Rajabu ni mwana wangu.
Tofauti katika uchopekaji wa viambajengo, sarufi geuzi huweza kuchopeka viambajengo katika sentensi na kuifanya sentensi hiyo kuwa tenda au tendwa. Kwa mfano, sentensi ya kauli ya kutenda inapogeuzwa na kuwa katika hali ya kutendwa kuna elementi ambazo huchopekwa.
Mfano; (a) Changwe anampiga mtoto
(b) Mtoto anapigwa na Alpha.
Hapa tunaona mofu {-w} na kihusishi {na} huchopekwa katika sentensi (a) na kuifanya sentensi hiyo kuwa ya kauli ya kutendwa katika (b). Ilhali sarufi miundo virai uchopekaji huo haujitokezi na hivyo kutokuonyesha mahusiano kati ya kauli tendi na tendwa.
Tofauti ya waasisi, sarufi geuzi iliasisiwa na mwanasarufi aitwaye Noam Chomsky (1957) ambaye anadai kuwa nadharia hii ya sarufi geuzi ilizuka ili kurekebisha taratibu za sarufi za awali. Yeye alidai kuwa sarufi za awali hazingeweza kuonyesha kuwa sentensi ya kauli ya kutenda na ile ya kauli ya kutendwa zinatokana na muundo mmoja wa ndani. Pia sarufi za awali hazingeweza kuonyesha mahusiano ya sentensi zinazotofautiana kwa ndani lakini ambazo zilikuwa na muundo wan je mmoja. Kwa mfano; Herman alinunuliwa shati na mwanawe.
Sura hii ya nje ya sentensi huwa ina sentensi kadhaa katika muundo wake wa ndani. Wakati sarufi miundo virai iliasisiwa na Bussmann (1996) ambaye anafafanua kwamba sheria miundo virai ni sheria zinazoonyesha mpangilio na ujenzi wa virai katika lugha, hivyo sheria hii huonyesha kuandikwa tena kwa viambajengo. Sheria kama,
S = KN+KT
yaani S = sentensi
KN = kikundi nomino/kirai nomino
KT = kikundi tenzi/kirai kitenzi
Inamaanisha kuwa sentensi inaweza kuandikwa kama Kikundi Nomino kikifuatwa na Kikundi Tenzi. Wakati mwingine sheria miundo virai huonyesha uhusiano wa utawazi hivi kwamba nomino hutawala Kikundi Nomino (KN). Kwa mfano sentensi kama; Amina ni mke wangu.
Suala la msingi ambalo wanaumuundo walisisitiza ni kutazama na kuchunguza lugha kisayansi. Hapa walisema kuwa masuala ilibidi yachunguzwe kwa uwazi na kuonyesha vitu, kategoria na elementi kwa uwazi zaidi. Ilhali sarufi geuzi hueleza ujuzi wa lugha ambao msemaji mzawa anao unaomwezesha kutumia lugha. Huu ni ujuzi wa kutunga sentensi kwa njia iliyo sahihi na vilevile namna sahihi ya kutamka na kueleza maana za maneno na sentensi. Mfano mmilisi wa lugha ya Kizinza anaweza kutunga sentensi zinazoeleweka na kutamka maneno ya lugha hiyo kwa usahihi kabisa.
Kwa ujumla, sarufi miundo virai na sarufi geuzi hufanana sana katika kuchunguza miundo ya lugha husika japo katika utendaji wake hujitokeza baadhi ya tofauti ambazo husababisha nadharia hizi za sarufi miundo kutofautiana katika vipengele kadha wa kadha kama vile uchopekaji wa viambajengo, maana zake pamoja na mfumo wa namna ya kuchanganua sentensi.
MAREJELEO
Habwe, J. & Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili.Nairobi: Phoenix Publishers.
Habwe, J. & Karanja, P. (2007). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili.Nairobi: Phoenix Publishers.
Kihore, Y.M. na wenzake. (2008). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: TUKI.
Massamba, D.P.B na Wenzake (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA); Sekondari na Vyuo. Dar es Saalam: TUKI.
Matinde, R.S. (2012). Dafina ya Lugha, Isimu na Nadharia; Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publishers (T) LTD.
Saluhaya, M.C. (2010). Nadharia ya Lugha Kidato cha Tano na Sita. Dar es Salaam: CHILDREN EDUCATION SOCIETY (CHESO).

Sunday, March 6, 2016

Muhadhara kuhusu Nadharia ya fonolojia zalishi na nadharia ya fonolojia asilia

Tofauti kati ya nadharia ya fonolojia asilia na nadharia ya fonolojia zalishi.
Nadharia ni mpango wa mawazo uliotungwa ili kuelekeza jinsi ya kufanya
au kutekeleza jambo Fulani (Mdee na wenzake, 2011 katika Matinde, 2012:247)
Massamba, D.P.B. (2004:64) anasema kuwa nadharia ni kanuni na misingi ambayo
hujengwa katika muundo wa kimawazo kwa madhumuni ya kutumiwa kama kiolezo ya kueleza
jambo. Kutokana na maelezo hayo tunaweza kusema kwamba nadharia ziliibuliwa na
wanafonolojia katika jitihada zao za kujaribu kuelewa na kufafanua sarufi majumui.
Kwa ujumla, nadharia huweza kufafanuliwa kama maelezo ya jambo yaliyofungamana
na vigezo vilivyowekwa au vilivyozalishwa kutokana na uchunguzi uliofanywa. Katika
utekelezaji wa uchunguzi wa jambo sharti mwanaisimu aongozwe na mwongozo maalumu
unaoogozwa na vigezo vilivyowekwa na wataalamu mbalimbali.
Nadharia za fonolojia ni mwongozo unaomuelekeza mwanaismu au mtu anayefundisha
fonolojia au mwanangenzi wa fonolojia kuifahamu fonolojia ya lugha katika vipengele vyake
vyote ili kujijengea utaratibu maalumu utakaomwezesha kuchunguza ubora na udhaifu
unaojitokeza katika nadharia nyingine za fonolojia. Katika uchanganuzi wa vipengele vya
kifonolojia lazima tuongozwe na mwongozo maalumu uliokubaliwa kwa vigezo vilivyowekwa
katika utekelezaji wa jambo hilo.Nadharia zijulikanazo katika uwanja huu wa fonolojia ni kama
vile fonolojia zalishi, fonolojia asilia, fonolojia zalishi asilia, fonolojia vipande sauti huru,
fonolojia umbo upeo, fonolojia mizani, fonolojia atomiki na fonolojia leksika.
Sababu za kuibuka kwa nadharia za fonolojia.
Kwanza, hakuna nadharia inayojitokeza katika ombwe bali nadharia yoyote mpya
itakuwa ama imeboresha nadharia iliyokuwepo hapo awali au inaikataa na kuipinga ile ya awali.
Katika uboreshaji wa nadharia ya awali ni muhimu kuelewa kwanza kipi kinafanyiwa maboresho
katika nadharia husika na kwa upande wa kupinga ni vyema kufahamu vipengele gani
vinapingwa na nadharia mpya katika nadharia ya awali kwa kutoa mifano kuntu.
Pili, si rahisi kuielewa nadharia mpya kinagaubaga bila kuielewa au kuzielewa nadharia
zilizotangulia kwani ubora na uelewa wa hiyo mpya unategemea kuielewa vizuri nadharia ya
awali.
Fonolojia zalishi ni mkabala wa kinadharia unaochunguza kanuni na sheria za
kimajumui zinazoonesha jinsi gani umbo la ndani na la nje yalivyokuwa yanahusiana
(Massamba, 2011:274). Waasisi wa nadharia ya fonolojia zalishi ni Noam Chomsky na Morris
Halle ambao wametililia mkazo katika uwepo wa umbo la ndani na umbo la nje katika
uwakilishi wa vipengele vya kifonolojia na kuonesha uhusiano uliopo baina ya maumbo haya.
Chomky na Halle wametoa sheria bunifu zinazo ongoza ukokotoajia wa maumbo hayo na kuziita
michakato ya kifonolojia. Fonolojia zalishi imechunguzwa na waasisi hao katika kitabu chao
maarufu kiitwacho Sound Pattern of English yaani “Ruwaza ya sauti katika lugha ya kiingereza
1968”. Fonolojia zalishi imejengwa na misingi ifuatayo:
(i) Maumbo na miundo yote ya lugha ya binadamu hutokana na umbo la ndani ambayo
hujengeka taratibu katika akili ya msemaji mzawa tangu anapoanza kujifunza lugha
akiwa mtoto mdogo mpaka anapopata umilisi kamilifu wa lugha yake.
(ii) Maumbo na miundo ya maneno tutamkayo katika vinywa vyetu huwakilisha umbo la nje
umbo ambalo kwa kiasi kikubwa huakisi umbo la ndani ama moja kwa moja au baada
ya kufanyiwa marekebisho kidogo.
(iii)Sauti zote zitumikazo katika lugha asilia za binadamu hutokana na mifumo ya
mkondohewa ambayo ama inakwenda ndani ya mapafu au inatoka nje ya mapafu ya
mzungumzaji. Mkondohewa hudhibitiwa na ala za matamshi katika jinsi na mahali pa
kutolewa au kuingia kwa hewa mapafuni.
Fonolojia asilia ni nadharia inayochunguza sulubu za sauti zitumikazo katika lugha ya
binadamu zilizomo katika maumbile ya binadamu yanayohusu usemaji na masikizi; kwamba
nguvu za kifonetiki katika sauti hujitokeza kupitia michakato ambayo inahusiana na
ubadilishanaji wa sauti katika akili na bongo zetu, Massamba (2011:117) Nadharia hii iliibuliwa
na David Stampe (1973) na baadaye kuungwa mkono na Donegan Patricia (1979). Pia
wanafonolojia hao wanatoa maoni kuwa michakato inayofanyika katika nadharia hii haitegemei
sheria wala kanuni bali huwa ni michakato asilia iliyo katika maumbile ya binadamu. Nadharia
hii iliibuka kushughulikia matatizo yaliyosababishwa na Kiunzi Rasmi cha Fonoloja Zalishi
kama vile udhahania na urasmi kanuni katika uwakikishi wa kifonolojia kwa malengo ya
kuboresha nadharia hiyo kwa kuifanyia marekebisho. Fonolojia asilia ina misingi ifuatayo:
(i) Fonolojia asilia inaelezea kipengele cha kifonoloja kama mwitikio asilia wa mahitaji,
uwezo na ulimwengu wa watumiaji wake.
(ii) Nadharia hii inaonesha hali halisi jinsi mambo yalivyo, kwa maana kwamba imekusudia
kuifafanua mada yake yenyewe.
(iii)Kipengele asili cha fonetiki katika fonolojia ni tofauti kabisa na kiengele cha kikaida cha
kifonetiki, kimaumbile, kimageuko, kisaikolojia na kiutokeaji wake.
(iv)Nguvu za kifonetiki katika sauti hujitokeza kupitia michakato ambayo inahusiana na
ubadilishanaji wa sauti katika akili na ubongo wa binadamu.
Tofauti kati ya fonolojia asilia na ile ya Chomsky na Halle (Fonolojia zalishi)
Kutokana na matatizo yaliyojitokeza katika Kiunzi Rasmi cha Fonolojia Zalishi (KRFZ), kuhusu
udhahania na urasmi kanuni wa uwakilishi wa vipengele vya kifonolojia, Davd Stampe na
Donegan Patricia waliibua nadharia ya fonolojia asilia (natural phonology) inayotofautiana na
nadharia ya fonolojia zalishi katika vipengele mbalimbali kama inaelezwa na Massamba(2011)
katika kazi yake ya Maendeleo Katika Nadharia ya Fonolojia.
Fonolojia zalishi hujikita katika kuelezea umbo la ndani na la nje ilhali fonolojia
asilia huelezea umbo la ndani tu. Fonolojia zalishi imejikita katika kuchunguza pamoja na
kuonesha uhusiano uliopo baina ya umbo la nje na umbo la ndani. Katika kuelezea hayo, waasisi
wa fonolojia zalishi walibuni mbinu mbalimbali au sheria na kanuni za ukokotoaji wa umbo la
nje kutokana na umbo la ndani, kwa mujibu wa TUKI (1990) wakinukuliwa na Matinde,
(2012:226) wanasema “Umbo la ndani katika taaluma ya sarufi geuzamaumbo zalishi ni
mshikamano dhahania wa vipashio vya tungo ambao ndio msingi wa tafsiri maana kamili ya
sentensi. Wanaendelea kusema umbo hili hujitokeza katika sentensi kabla sentensi haijafanyiwa
mageuzi yoyote. Pia Matinde, (2012:226) anasema “umbo la nje hutokea baada umbo la ndani
kufanyiwa marekebisho au mageuzi muhimu hadi kufikia kiwango cha usemaji sahihi na
unaokubalika.” Umbo hili kwa mujibu wa Matinde hudhihirika kimatamshi na kiothografia
(kimaandishi). Kinyume na ilivyo katika fonolojia asilia ambayo hujikita zaidi kuelezea umbo la
ndani tu. Kwa mfano katika katika badiliko la vokali kuwa nusu vokali.
[u]----- [w]/--- [v] (isiyo [u])
Ikiwa na maana kuwa [u] hubadilika kuwa nusu irabu [w] katika mazingira ya kutanguliwa na na
irabu isiyo [u] yenyewe, katika maneno haya:
Umbo la ndani                                   Umbo la nje
Muana                                                  Mwana
{Mu+a+na}                            
Mualimu {Mu+alimu}                            Mwalimu
Muema {Mu+ema}                                Mwema
Hivyo umbo la nje hutokea baada ya mchakato wa ukokotozi katika umbo la ndani na kupelekea
kuzaliwa kwa umbo hilo.
Waasisi wa fonolojia zalishi wanaaminin kwamba mabadiliko ya kifonetiki ni suala
la kujifunza ilhali waasisi wa fonolojia asilia wao huamini mabadiliko hayo si ya kujifunza.
Katika fonolojia zalishi, Chomky na Halle wanaamini kwamba mabadiliko ya kifonetiki ni suala
la kijifunza. Hii ina maana kwamba mabadiliko ambayo yanatokea katika sauti mbalimbali za
binadamu, mtu hujifunza ili kuyaelewa mabadiliko hayo mfano wa mabadiliko ni kama vile
ukaakaishaji, tangamano la irabu, mvutano wa irabu, kudhoofika na kuimarika kwa fonimu na
mengnine lakini katika fonolojia asilia Stampe na Donegan waanaamini kwamba mabadiliko
hayo mtu hajifunzi bali ni mwitikio asilia wa nguvu za kifonetiki za kutoa na kuingiza ambazo
zimo katika uwezo alionao binadamu katika kuelewa usemaji.
Katika fonolojia zalishi mtoto ana sheria nyingi kuliko mtu mzima lakini katika
fonolojia asilia hizi si sheria bali ni michakato asilia ambayo inachombezwa na uthibiti
anaozaliwa nao mtoto uliomo katika umbo la kifonetiki. Katika fonolojia zalishi hii inatokana
na kwamba mtoto anapozungumza na mtu mzima hutumia umbo la ndani ambalo kwa wana
fonolojia zalishi ili kupata umbo la nje lazima kuwe na sheria maalumu ya kupata umbo la nje na
hapo ndipo mtoto huzalisha sheria nyingi zaidi. Kwa mfano, katika badiliko hili la kudhoofika
kwa fonimu
[d] ---- [z]/---- [i]
Ikiwa na maana kuwa sauti [d] hubadilika kuwa sauti [z] katika mazingira ya kutanguliwa na
vokali [i] katika neno haya:
Umbo ndani          Fonimu dhoofika   Umbo la nje 

Mpendi                            [d--- z]            Mpenzi

Mlindi                               [d--- z]            Mlinzi                                                                                            Mpandi                            [d--- z]            Mpanzi 

 Lakini kwa upande wa fonolojia asilia wao kwao hizo si sheria bali ni michakato asilia ambayo
inachombezwa na uthibiti anaozaliwa nao mtoto uliomo katika umbo la kifonetiki.
Lengo la fonolojia zalishi ni kuchunguza umilisi wa lugha halisi lakini fonolojia
asilia inaamini kuwa hiyo siyo lugha halisi kwani kwa kufanya hivyo unaichunguza lugha
hiyo kimajumui. Chomsky na Halle wanaamini kwamba lengo la mwanaisimu ni kuchunguza
umilisi wa lugha alionao binadamu kama lugha yake halisi. Mtu anapokuwa na umilisi wa lugha
atakuwa anatumia sauti ambazo zinakubalika katika lugha yake na hiyo ndiyo lugha halisi kwake
lakini wanafonolojia asilia wanasema unapochunguza lugha katika umilisi utakuwa unachunguza
lugha hiyo kimajumui katika masuala ya kifonetiki kwa hiyo mwelekeo wa mawazo yao ni kuwa
hiyo si lugha halisi. Ingawa Stampe na Donegan hawajatuonesha kuwa lugha halisi ni ipi lakini
mawazo yao yanaelekea katika mtazamo kwamba lugha halisi ni lugha ambayo hutumiwa na
mtoto kabla hata kupata umilisi wa lugha hiyo anayoitumia.
Fonolojia zalishi iliegemea zaidi katika urasimi wa mashartizuizi ilhali fonolojia
asilia haina mashartizuizi ambayo ni rasmi kwani yenyewe si nadharia ya kikaida.
Fonolojia zalishi inafuata taratibu, kanuni na sheria mbalimbali katika kuunda na kuzalisha
maneno mbalimbali ambayo ni lazima kuwepo na sheria rasmi zinazokokotoa umbo la ndani
kwenda umbo la nje. Kwa mfano, katika badiliko la mvutano wa irabu wumbo la ndani la neno
Juu mbele |i| + chini kati |a|------ mbele kati |e|
Ikiwa na maana kuwa irabu ya mbele juu |i| huvutana na irabu ya chini kati |a| na kuunda irabu
mbele chini |e| katika maneno haya:
Umbo la ndani                     Umbo la n je
Maino (ma+ino)                        Meno
Waizi (wa+izi)                           Wezi
Waingi (wa+ingi)                       Wengi
Maiko (ma+iko)                         Meko
katika lugha ya Kiswahili badiliko hili limetokana a na sheria na si kinasibu tu. Katika badiliko
hili, irabu ya juu mbele |i| huvutana na irabu ya chini kati |a| na kuunda irabu ya mbele kati |e|.
kwa upande wa nadharia ya fonolojia asilia si ya kikaida kwa sababu imekusudia kuifafanua
mada yake yenyewe na kwa kufanya hivyo inaonesha kwamba nadharia hii inaonesha hali haisi
jinsi maumbo ya maneno yalivyo.
Katika fonolojia zalishi fonimu ya mtoto hukua hatua kwa hatua kadri anavyozidi
kutambua ukinzani wa sauti ilhali katika fonolojia asilia huwa kuna usawazishaji wa
fonimu hizo. Kwa mfano, katika fonolojia zalishi mtu ambaye hajabalehe katika lugha hutamka
fonimu ambazo hazijakomaa kama vile:
(i) Ugali vamvu badala ya ugali kisamvu
(ii) Mama omba mma kunya badala ya mama naomba maji ya kunywa.
(iii) Nataka jojoa badala ya nataka kukojoa
Mtoto hutumia sauti hizo kwasababu bado hajatambua matumizi sahihi.Lakini kwa upande wa fonolojia asilia kuna ukinzani wa sauti hizo lakini kadrianavyozidi kuwa mkubwa anaanza kuthibiti ukinzani huo kwa kuanza kutumia sautizinazoelekea kuwa sahihi hadi kuthibiti ukinzani huo vizuri. Kwa upande wa fonolojia asiliafonimu hizo hazikui hatua kwa hatua bali nai usawazishaji wa matamshi ambao unakaribaina nawa mtu mzima, sauti hizo husawazishwa kulingana na zile za watu wazima hadi zile tofauti zakimatamshi zitakapopotea kulingana na fonimu ya mtu mzima.
Hivyo basi, mapinduzi yaliyoletwa na Chomky na Halle katika uwanja wa fonolojia
yalikuwa ni makubwa sana lakini wanazuoni wa fonolojia waliibuka na kuona kuwa mabadiliko
hayo yamekuwa na matatizo mawili, kwanza udhahania, pili urasimi kanuni katika uwakishaji
wa vipengele vya kifonolojia. Madai hayo yalipelekea kuibuka kwa mikabala mingine ya
kinadharia kuelezea jinsi ya kuondokana na matatizo hayo na baadhi ya mikabala hiyo
ilionekana kupinga kabisa na mingine kuboresha kiunzi rasmi cha fonolojia zalishi. Mojawapo
ya mkabala wa kinadharia ulioiburiwa ni fonolojia asilia ambayo inachunguza sulubu za sauti za
binadamu zinazojikita katika usemaji na masikizi, kwa kuangalia zaidi umbo la ndani ambalo
hubadilika kuwa umbo la nje. Pia ieleweke kwamba Chomky na Halle hawakubuni uhusianao wa
umbo la ndani na umbo la nje bali wao walikuja kuelezea sheria na michakato inayofanyika
katika kuunda umbo la nje ambalo kwa kiasi kikubwa huaksi umbo la ndani. Sheria walizozibuni
kuelezea fonolojia majumui ni pamoja na michakato ya kiusilimisho (assimilatory processes) na
michakato isousilimisho (non-assimilatory processes).


                  



                                                MAREJELEO
Massamba, D.P.B. (2011). Maendeleo Katika Nadharia ya Fonolojia. Taasisi ya Taaluma za
Kiswahili chuo Kikuu cha Dar es salaam. Dar es salaam: TUKI.

Massamba, D.P.B. (2004). Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA), Sekondari na Vyuo.
Dar es salaam. TUKI

Matinde, R.S. (2012) Dafina ya lugha, Isimu na Nadharia Sekondari Vyuo vya kati na vyuo
Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publisher (T) Ltd.

                                                                                   PONGEZI

                                                                           Kwa Enlightenment group

                                                                                  SAUT-Mwanza.

                                                                                     (2013/2016)













hakiki na tuma maoni au mapendekezo kuhusu makala hii ya andiko langu la uchunguandiko langu

ANDIKO LA UCHUNGU (Kwa shemeji zangu na wanangu)           NYAMBUYA OGUCHU,                            S.L.P 777666,       ...